Timu ya taifa ya Crotia jana ilibuka kifua mbele kwenye kundi D baada ya kuifunga Hispania mabao 2-1 kwenye dimba la Bordeaux.
Spain ilipata bao la kuongoza kupitia Alvaro Morata kwenye kwenye dakika ya 7 ya mchezo ambapo Nikola Kalinic alichomoa bao hilo kwenye dakika ya 45 kipindi cha kwanza na baadae Ivan Perisic alifunga la pili kwenye dakika ya 86.
Matokeo hay yanaifanya Crotia kuongoza kundi kwa pointi 7, ikifuatiwa na Hispania yenye pointi 6, Uturuki yenye pointi 3 na Jamuhuri ya Czech yenye pointi moja.
Sergio Ramos ambaye ni nahodha wa Hispania alikosa penati kwenye mechi na kuikosesha nafasi timu yake kuongoza kundi hilo.

Comments
Post a Comment