Brazil imemfukuza kazi kocha wao Carlos Dunga baada ya timu hiyo kufanya vibaya kwenye michuano ya Copa America Centenario inayoendelea nchini Marekani.
Brazil imefikia uamuzi huo baada ya timu hiyo kufanya vibaya kwenye hatua ya makundi ambapo ilipata sare dhidi ya Ecuador, kushinda dhidi ya Haiti goli 7-1, kupoteza kwa Peru goli 1-0 na kuifanya timu hiyo ifunganshe virango vyake.
Nafasi ya Dunga itachukuliwa na Tite ambaye ni kocha wa Corithians atakayeiongoza timu hiyo kwenye michauno ya Olympic.

Comments
Post a Comment