Timu ya Taifa ya England ili kubali kuvutwa shati na timu ya Urusi baada ya kukubali matokeo kuwa 1-1 hadi mwisho wa mchezo.
England ilipata bao la kuongoza kupitia Eric Dier ambaye alifunga kwa shuti kali kutokana na adhabu ndogo nje ya lango la timu ya Urusi hata Hivyo Urusi ilichomoa bao kwenye dakika ya 90 ya mchezo kupitia Berezutski aliyefunga kwa kichwa.
Licha ya matokeo hayo ya sare lakini England ilichezea nafasi nyingi za wazi kutokana na kutawala zaidi mchezo katika kipindi cha kwanza.
Hata hivyo imani ya kocha ya Roy Hogdson kwa baadhi ya wachezaji ilichangia kwa kiasi kikubwa England kupoteza mchezo huo.

Comments
Post a Comment