England yasimama nyuma ya Wales


Timu ya England imeshindwa kufua dafu mbele ya Wales baada ya kushindwa kuongoza kundi hilo kutokana na matokeo ya sare dhidi ya Slovakia.

Wales ilishinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Urusi kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na Aaron Ramsey ambaye alifunga bao la kwanza, Neil Taylor aliyefunga la pili na Gareth bale aliyefunga la tatu.

Pamoja na England kufuzu huenda ikaangukia katika timu ngumu kwenye hatua ya mtoano kutokana na timu nyingi bora kuongoza makundi yao.

Katika kundi Wales ameongoza kwa pointi 6, ikfuatiwa na England yenye pointi 5, Slovakia 4 na Urusi ikiwa na pointi 1.

Comments