Bailly 22, anafukuziwa na timu mbalimbali ikiwemo Manchester city, Barcelona na Paris Saint-Germain lakini hadi sasa Manchester united inaongoza kwenye mbio za kumsajili Beki huyo.
Manchester united huenda ikamwaga mzigo wa euro 31 milioni ili kumaliza zoezi la kumsajili beki huyo baada ya makubaliano baina yao na villareal kufikia kwenye dau hilo.
Bailly alisajiliwa na Villareal akitokea Espanyol kwa dau la euro 5 milioni 2015 January baada ya Villareal kumuuza beki wao kati Gabriel Paulista kuelekea Arsenal.

Comments
Post a Comment