Kiungo wa timu Borussia Dortmund Ilkay amekuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Pep Gurdiola baada ya kumwaga wino Etihad.
Gundogan amesaini mkataba wa miaka minne wenye thamani ya Euro 21 milioni kuitumikia Manchester city.
"Najisikia faraja kujiunga na Man city, Gurdiola aliongea na mimi kwa kirefu kuhusiana na safari yangu ya kutua hapa.
"Kuna changamoto kubwa kuichezea ligi ya Uingereza na timu kubwa kama Man city lakini nina furaha kuwa nao." Alisema Gundogan

Comments
Post a Comment