Hans: Simba mambo safi


Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Zacharia Hans Pope amesema kuwa timu yake inasajili kwa raha kwa kuwa haina presha.

Zacharia alisema kuwa Simba haina cha kupigania dhidi ya Yanga hivyo hawaoni sababu ya kuweka presha ya Usajili badala yake wamejikita kwenye hatua za msingi ili kufanya usajili ulio bora.

"Kama kuna mchezaji Yanga ilimlenga kwa ajili ya Usajili hakuwa kwenye mipango yetu, hatuhitaji wachezaji wanaowahitaji, tuna mipango yetu nje ya Yanga na Azam." Alisema mwenyekiti huyo

Zacharia aliongeza kuwa bado wanaendelea na mipango ya kufanya mazunguzo na baadhi ya wachezaji wanaohtaji kuwasajili ndani na nje ya Tanzania.

Comments