Hans: usajili Simba kiboko


Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa timu ya Simba Zacharia Hans Poppe amesema kuwa usajili ulifanywa na kamati yake katika timu hiyo ni babu kubwa.

Hans alisema kuwa kwa sasa wana andaa timu ya ushindani ambayo itarejesha furaha kwa mashabiki wa Simba na kuiletea timu hiyo kongwe Heshima yake.

"Tunajipanga kuhakikisha tunakuwa na timu bora, kufungwa na Yanga ilituumiza sana sisi na mashabiki lakini tunatoa ahadi jambo hilo halitajirudia." Alisema Hans

Simba tayari imekalisha usajili wa wachezaji akiwemo Mohamed Ibrahimu na Muzamil Yasin wote kutoka mtibwa, Juma Mnyate na Emanuel Semwaza wote  kutoka Mwadui.

Comments