Bodi ya ligi ya (TLBP) ya shirikidho la soka la Tanzania TFF limetangaza makundi matatu ya timu zitakazoshiriki ligi daraja la kwanza ya star times msimu wa 2016//17.
ligi hiyo inatarajiwa kuanza agosti mwaka huu mara baada ya shirikisho hilo kukamilisha mchakato wa usajili timu hizo utakaoanza Juni 15 mwaka huu.
Bodi hiyo imepanga makundi matatu yanayoshirikisha timu 8 mabayo yamegawanywa katika alama A, B na C Ambapo mgawanyiko umepangwa ifuatavyo
Kundi A inazishirikisha timu zifuatazo ikiwemo Abajalo ya Dar es Salaam, African sports, Ashanti United, Kiluvya united ya pwani, Friends Rangers ya Dar es Salaa, Lipuli ya Iringa, Mshikamano FC ya Dar es Salaam na Polisi ya Dar es salaam.
Wakati kundi zipo Jkt mlale ya Ruvuma, Coastal Union ya Tanga, Kimondo FC ya Mbeya, Kinondoni Municipal Council ya Dar es salaam, Kurugenzi ya Iringa, Mbeya worriors ya Mbeya, Njombe mji ya Njombe na Polisi ya Morogoro.
Na kundi C, ipo ya Alliance schools ya Mwanza, Mgambo Shooting ya Tanga, Mvuvumwa FC ya kigoma, Panone FC ya Kilimanjaro, Polisi Dodoma ya Dodoma, Polisi Mara ya Mara, Rhino Rangers ya Tabora na Singida united ya Singida.

Comments
Post a Comment