Hii ndiyo barua ya TFF kwa Muro


Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limemfungulia malalamiko Msemaji wa timu ya Yanga Jerry Muro kwa baada ya kupingana na maamuzi ya chama hicho pamoja kuwashambulia wenye vyombo vya habari.

TFF imemtaka Jerry Muro kufika mbele ya kamati itakayokutana siku Julai 2, mwaka huu majira ya saa nne na nusu asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizopo kwenye ofisi za TFF karume.

Katika barua hiyo inaonesha kuwa Jerry Muro ana hiari ya kufika mwenyewe na kufanya utetezi wake kwa matamshi ya kinywa chake, kupeleka barua au kutuma mwakilishi.


Barua ya TFF kwa Jerry Muro

Mara kadhaa msamaji huyo wa Yanga ameingia kwenye marumbano na baadhi ya wahusika wa timu kadhaa akiwemo msemaji wa Simba Haji Manara.

Comments