Timu ya Yanga leo imetoa rasmi kalenda yake ya matukio ya uchaguzi na kuitaka TFF isiwaingilie kwenye mchakato huo.
Yanga ambayo itafanya uchaguzi wake mkuu Julai 11 mwaka huu imetangaza leo nafasi zitakazogombewa katika uchaguzi mkuu huku zoezi la kuchukua fomu za kugombea litafanyika kwa siku mbili kati ya tarehe 2 na 3 mwezi Juni mwaka huu.
kuanzia Juni 4 mwaka huu timu hiyo itaanza kufanya mchujo wa awali kwa wagombea na kuchapisha majina ya wagombea rasmi kwenye ubao wa matangazo na kati ya Juni 5 timu hiyo itapokea pingamizi kwa wagombea mbalimbali na kusikikiliza rufaa pamoja na kutoa maamuzi kati ya Juni 6 hadi 7.
Aidha Yanga imeidhinisha wagombea wa nafasi mbalimbali za uchaguzi kufanya kampeni na kunadi sera zao ifiikapo julai 7hadi 10 mwaka huu baada ambapo Julai 11 uchaguzi utafanyika.
Hata hivyo Yanga imeweka wazi kwenye kalenda kwenye hiyo ya matukio kuwa matokeo ya uchaguzi huo yatatangazwa rasmi Julai 12 mwaka ikiwa ni siku moja kupita baada ya uchaguzi mkuu.

Comments
Post a Comment