Mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden Zlatan Ibrahimovic anatarajiwa kukamilisha zoezi la vipimo katika timu ya Manchester united wiki ijayo.
Ibrahimovic tayari amefanya makubaliano binafsi na timu ya Manchester united wakati akiendelea na michuano ya UEFA Euro kabla ya kutolewa kwa timu yake.
Mchezaji huyo ana mahusiano mazuri na kocha Jose Mourinho tangu Intermilan wakati kocha huyo wa Man united alipokuwa akiwanoa waitaliano hao.
Tayari Mourinho anaonekana kukamilisha mipango yake aliyoiweka baada ya Ibrahimovic kukubali kusaini mwaka mmoja kuitumika Manchester united.

Comments
Post a Comment