Timu ya Yanga imevunja mkataba na kiungo wao Issofou Boubacar kutokana na kutoridhishwa na kiwango chake.
Yanga ilimpatia Issoufou barua yake ya kumvunja nae mkataba saa chache baada ya kumpa mkataba mpya mkongomani Mbuyu Twitte.
Twitte alisaini miaka miwili mbele ya kuendelea kuitumikia Yanga kutokana na juhudi zake za kuweza kucheza namba tofauti kwenye timu hiyo.
Yanga inaendelea na mkakati wa kusaka nyota wapya kwa ajili ya kuongeza nguvu na kuimarisha kikosi chao hadi kufikia jana tayari Andrew Vicent wa Mtibwa Sugar alikua ashasaini miaka miwili kwa wana jangwani hao.

Comments
Post a Comment