Timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imepoteza mchezo wa leo baada kufungwa mabao 2-0 na timu ya taifa ya Misri.
Mchezaji wa AS Roma Mohamed Salah ndiye aliyefunga mabao yote mawili baada ya kufunga la kwanza katika dakika ya 45 na kuzamisha lingine la pili dakika ya 58 ya mchezo.
Stars imepoteza rasmi nafasi ya kushiriki fainali hizo za mataifa Afrika nchini Gaboni baada ya kuruhusu kipigo hicho nyumbani ikiwa ni kipigo cha pili baada ya kupoteza mechi ya kwanza nchini Misri.
Salah amewahi kuichezea FC Basel ya Uswisi, Chelsea ambayo ilimtoa Fiorentina kwa mkopo na sasa anaichezea Roma ya Italy na amekuwa nyota wa timu hiyo.

Comments
Post a Comment