Joe Allen kurejea Swansea


Kiungo wa timu ya Liverpool Joe Allen huenda akarajea kwenye timu yake ya zamani Baada ya Swansea kufikia pazuri kwenye dili hilo.

Swansea imeweka mezani dau la euro 10 milioni ili kufanikisha mpango wa kumrudisha kiungo huyo ambaye amepoteza namba kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Jurgen Klopp.

Kocha wa zamani wa Liverpool Brendan Rodgers ndiye aliyemsajili kiungo huyo mwaka 2012 muda mfupi baada ya kocha huyo kuachana na timu ya Swansea.

Allen 26, kwa sasa yupo na timu ya taifa ya Wales kwenye michuano ya EUFA euro inayoendelea nchini Ufaransa lakini dili linaweza kukamilika hivi karibuni.

Comments