Juma Abdul aanza mazoezi


Beki wa kulia wa timu ya Yanga Juma Abdul ameanza mazoezi ya taratibu baada ya kukaa nje ya uwanja kwa wiki moja.

Juma Abdul hakuweza kuungana na Yanga ambayo imeweka kambi yake nchini Uturuki kutoka na majeraha na huenda akarejea dhidi ya Mazembe baada ya kuanza mazoezi.

Yanga ilipoteza mchezo dhidi ya MO Bejaia ya Algeria baada ya kufungwa Goli 1-0 katika mchezo wa kwanza ambao Yanga ilicheza kwenye kundi hilo.

Juma Abdul anafanya mazoezi ya taratibu chini ya uangalizi wa daktari huenda akarejea tena kikosini kulingana na ripoti za daktari huyo.

Comments