Juventus yamtolea macho Benteke


Timu ya Juventus inataka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Christian Benteke ambaye amekosa namba ya kudumu tangu atue Anfield.

Juventus ina wasiwasi huenda isibaki na mshambuliaji wao mahiri Avaro Morata ambaye amekuwa akiwaniwa na timu kadhaa ikiwemo Arsenal, Chelsea, Manchester city na Real Madrid na hivyo wanaona Benteke ni mshambuliaji Sahihi kuziba pengo hilo.

Real Madrid inaongoza kwenye mbio za kumrudisha Morata Bernabeu na yeye anavutika na timu yake ya zamani jambo linaloisukuma Juventus kuingia vitani na Chelsea kumwania Christian Benteke.

Licha ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza Livepool, Benteke 25 amefunga magoli 9 katika mechi 29 alizoicheza akiwa na timu hiyo.

Comments