Kally Ongala ataendelea kuwa kocha wa timu ya Majimaji ya Songea baada ya uongozi wa timu kumpa mkataba mpya wa kuendelea kuwanoa wana lizombe.
Mwenyekiti wa timu hiyo Humphrey Milanzi alisema kuwa kwa sasa wameshamaliza na kocha huyo na wanafikiria suala zima la usajili ili kutengeneza timu ya ushindani itakayofanya vizuri kwenye ligi.
"Tumefurahi baada ya kufikia makubaliano na kocha wetu, tumempa mkataba wa mwaka mmoja, tunamtakia kila kheri." Alisema Milanzi\
Ongala alikabidhiwa timu hiyo ikiwa mkiani baada ya kufanya vibaya kwenye mechi 13 za mwanzo, na baadae aliinyanyua timu hiyo ambayo ilimaliza nafasi ya kumi baada ya kukusanya jumla ya pointi 35 kwenye ligi.

Comments
Post a Comment