Wachezaji wawili waliosajiliwa Yanga Hassan Kessy pamoja na Andrew Vicent 'Dante' wameanza rasmi mazoezi na timu hiyo kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Kessy na Dante wameingia wakiwa na hali mpya kwenye timu baada kuonekana wakifanya mazoezi kwa moyo na kujituma huku wakifuata vema maelekezo ya mwalimu Hans Pluijm.
Kessy aliachana na Simba ambayo haikuonesha nia ya kumpa mkataba mpya baada ya mkataba wake kuelekea ukingoni ambapo alichukua uamuzi wa kusaini Yanga.
Yanga imefanya marekebisho kadhaa kwenye timu yao ikiwemo kuwaongezea mkataba baadhi ya wachezaji kusajili wengine akiwemo Adrew Vicent kutoka Mtibwa Sugar na Juma Mahadh wa Coastal union.

Comments
Post a Comment