King Messi astaafu timu ya taifa


Mshambuliaji nyota wa timu ya Barcelona ameamua kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya Argentina muda mfupi baada ya mchezo wa fainali dhidi ya Chile.

Messi ameshindwa kutwaa taji lolote akiwa na Argentina ambapo kufikia jana nyota huyo bora duniani aliamua kutangaza rasmi kuachana na soka la kimataifa.

"Nilitamani kufikia mafanikio na timu ya taifa, nimejaribu ninavyoweza nimetokea kushindwa mara kadhaa, nadhani sasa nastahili kupumzika." Alisema Messi.

Chile imetetea kwa mara ya pili mfululizo ubingwa wa Copa America ikiwa ni mara ya pili mfululizo kuing'oa Argentina kwenye fainali hizo.

Chile iliing'oa Argentina kwa mikwaju ya penati na sasa mabingwa hao wamefungua mlango wa kustaafu kwa nyota wa huyo dunia akiwa na miaka 29.

Comments