Liverpool yakubari dau la Hector


Timu ya Liverpool imeruhisiwa kufanya mazunguzo na mchezaji wa FC Cologne Jonas Hector baada ya kukubali dau la uhamisho.

Wakala wa mchezaji huyo alisema kuwa Liverpool imekubali kutoa kiasi cha euro 12 milioni ili kufanikisha usajili wa mchezaji huyo.

Hector 26, ana uwezo mkubwa wa kucheza beki ya kushoto na beki wa wakati na ameonesha uwezo mkubwa kwenye ligi ya Bundesliga jambo pekee linalomvutia Jurgen Klopp kukamilisha dili hilo.

Klopp anaona ni wakati huu ambao beki mspaniola Alberto Moreno kupokea changamoto ili kuijenga Liverpool yenye ushindani pande zote.

Hector kwa sasa yupo na kikosi cha timu ya taifa ya Ujermani ambacho kitashiriki michuano ya UEFA euro nchini Ufaransa itakayoanza Juni 10 mwaka huu

Comments