Maguri apata shavu Oman


Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Simba Elias Maguli amepata shavu la kucheza soka kwenye ligi ya Oman baada ya kusaini miaka mitatu kuitumia Dhofar SC.

Maguri ambaye ana uwezo mkubwa kufumania nyavu alisaini mkataba huo jana na sasa macho ya watanzania watamwona mchezaji huyo endapo ataungana na timu ya taifa.

Maguri alionesha kiwango bora alipokuwa na Stand united licha ya mara kadhaa mwalimu Patrick Liewing kumweka benchi lakini bado amekuwa na uwezo mkubwa wa kufumania nyavu.

Maguri alitupia nyavuni magori 15 kwenye ligi ya Vodacom iliyopita akiwa nyuma ya Hamis Tambwe aliyefunga magoli 21, Hamis Kiiza pamoja na Donald Ngoma.

Comments