Mshambuliaji wa zamani wa Simba ambaye sasa anakipiga katika timu ya Stand United amesema anaweza kurejea Simba endapo itampa mkataba.
Maguri alisema kuwa anatanguliza mbele kazi yake kuliko mambo mabaya yaliyowahi kutokea baina yake na Simba na sasa yupo tayari kuitumikia kwa mara nyingine.
Mshambuliaji huyo ambaye alifunga goli 15 msimu huu amekuwa kwenye wakati mzuri akiwa na Stand united pamoja na Taifa Stars na wakati huu huenda Simba ikamuhitaji kwa mara nyingine kutokana na kiwango bora alichonacho.
"Kama Simba ipo tayari inipe mkataba, kwa sasa nipo tayari kuisikiliza timu yoyote itakayohitaji huduma yangu." Alisema Maguri
Maguri aliwahi kuichezea Simba msimu wa 2014/15 na kuelekea Stand united ambapo kwa sasa amemaliza mkataba wake na timu hiyo.

Comments
Post a Comment