Majabvi akubali kubaki Simba

Kiungo wa Simba Justice majabvi amekubali kuendelea kuitumikia timu hiyo baada ya kufanya maongezi na viongozi wa timu

Awali Majabvi ambaye ni raia wa Zimbabwe alisema kuwa ataungana na mkewe aliyehamishwa kikazi nchini Australia na kuachana na timu hiyo.

Majabvi ambaye hucheza nafasi ya kiungo na beki wa kati katika timu ya Simba amekuwa nguzo tangu atue msimbazi na wakati wote amekuwa kwenye kiwango cha hali juu.

Licha ya Simba kuwa na mipango ya kuwaacha baadhi ya wageni lakini iliumia kichwa namna kumbakisha kiungo huyo ambaye huyo ambaye sasa analeta matumaini mapya kwa wanamsimbazi.

Comments