Makabe Veterans yafanya ziara ya kimichezo Moshi


Klabu ya Makabe Veterans leo imeondoka kuelekea Moshi kufanya ziara yake ya kimichezo kwa siku mbili.

Makabe Veterani chini ya kocha wao Isack Kibanga itashuka dimbani kesho katika mchezo wa kujipima Nguvu dhidi ya TPC Moshi na timu ya Ushiriki ambao ndiyo wenyeji.

Viongozi na wachezaji wa makabe veterans 

Licha ya ziara hiyo ya kuelekea Moshi klabu hiyo imewahi kufanya ziara zake mbalimbali katika mikoa tofauti  ya Tanzania ikiwemo Morogoro, Arusha na Tanga ikiwa na lengo kukuza uhusiano baina ya timu hiyo na veterans vingine Tanzania.

Isack Mwang’onda mwenye t-shirt ya pundamilia ndiye mwenyekiti wa timu hiyo


Comments