Timu ya Liverpool inajiandaa kuweka mezani dau la euro 30 milioni ili kuinasa saini ya mshambuliaji wa southampton Sadio Mane.
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amefikia uamuzi huo baada ya kiungo wa Bayern Munich Mario Gotze kukataa kujiunga na majogoo hao wa Anfield tangu kuondoka kwa Pep Gurdiola.
Mane ambaye alitokea Redbull Salzburg ya Austria amekuwa nguzo muhimu katika timu ya Southampton na tangu atuekwenye timu hiyo amekuwa gumzo kwa mabeki wa England.
Kulingana na mfumo wa Klopp unaotumia kasi kubwa uwanjani anaona Mane ni mbadala sahihi wa Mario Gotze ili kutengeneza timu ya ushindani katika msimu 2016/17.
Liverpool imeamua kufikia dau baada ya Southampton kukataa ofa ya kwanza ya euro 20 milioni na huenda wakafanikiwa kuinasa saini ya mchezaji huyo ambaye ni raia wa Senegal.

Comments
Post a Comment