Mane anukia Liverpool


Nyota wa timu ya Southampton Sadio Mane huenda akatua Liverpool muda wowote kuanzia sasa baada ya dili hilo vizuri.

Liverpool imekubali kutoa dau la Euro 30 Milioni kama ada ya uhamisho wa mchezaji huyo ambayo ilipangwa na timu ya Southampton.

Mane 24, amekuwa kwenye kiwango bora tangu asajiliwe na Southampton akitokea Redbull Salzburg ya Austria ambapo akiwa na huko alifunga magoli 10 kwa msimu.

Endapo dili hilo litakamilika Sadio Mane atakuwa ni mchezaji wa tatu kuwahi kusajiliwa kwa Gharama na Liverpool baada ya kufanya kwa Andy Caroll kwa dau la Euro 35 milioni akitokea Newcastle na Christian Benteke Euro 32 Milioni akitokea Aston Villa.

Comments