Timu ya Liverpool imekamilisha usajili wa Sadio Mane wa Southampton baada ya winga huyo kumwaga wino Anfield.
Mane 25, amesaini mkataba wa miaka mitano utakaomweka Liverpool hadi mwaka 2021 kwa dau la euro 34 milioni kama ada ya uhamisho
Winga huyo amedumu Southampton kwa miaka 2 na kuifungia Saints idadi ya mabao 25 katika mechi 75 aliyoichezea timu hiyo.
Dau la uhamisho la euro 34 milion kunamfanya mane kuingia kwenye orodha ya wachezaji waliosajiliwa kwa gharama kubwa baada ya Ken Daglish kufanya hivyo kwa Andy Caroll.
Comments
Post a Comment