Michy Batshuayi afanyiwa vipimo Chelsea


Mshambualiaji nyota wa timu ya taifa ya Ubelgiji Michy Batshuayi amefaulu zoezi la vipimo baada kwenye timu ya Chelsea baada ya kufanyika kwa zoezi hilo jana.

Batshuayi aliondoka kwenye kambi ya Ubelgiji kuelekea Bordeaux ambako alikutana na daktari wa Chelsea ambaye alimfanyia vipimo nyota huyo ili kukamilisha dili lake la kutua Stamford Bridge.

Mshambuali huyo wa Merseille alifunga jumla ya magoli 17 msimu uliopita katika katika ligi ya Ufaransa maarufu kama 'league 1'.

Mbali na Chelsea nyota huyo mwenye thamani ya Euro 33 milioni anazitoa macho baadhi ya klabu ikiwemo Crystal Palace na West Ham ambao wapo tayari kutoa dau hilo.

Comments