Nahodha wa timu ya taifa ya Crotia Darijo Srna ameachana na fainali za kombe la mataifa barani Ulaya baada ya kupokea taarifa za kifo cha baba yake mzazi.
Beki huyo wa kulia anayekipiga katika timu ya Shakhtar Donetsk atahudhuria mazishi hayo baada ya kucheza dakika 90 katika mchezo ulipigwa jana dhidi ya Uturuki ambapo walishinda goli 1-0.
Chama cha soka nchini Crotia kilithibitisha taarifa za kifo cha baba mzazi wa mchezaji mwenye miaka 34 na kuandaa mkakati wa kutuma salamu za rambirambi kwa familia yake..
wachezaji wenzake waliobaki kwenye kikosi cha Crotia waliandika katika ukarasa wa Twitter wako pamoja naye yeye na familia yake.

Comments
Post a Comment