Arsenal na Liverpool ndizo zitakazofungua mtanange wa ligi kuu kwenye uwanja wa Emirates uingereza ifikapo Agosti 13, mwaka huu ikiwa ni mechi ya kwanza kuleta mwamko wa mashabiki wa ligi hiyo duniani.
Ligi hiyo itakaribisha London derby kati ya Chelsea na wagonga nyundo wa London 'West Ham' katika wiki ya ufunguzi ambapo mashabiki wengi wa Chelsea hamu yao ni kuona mambo mapya chini ya Muitaliano Antonio Conte ambaye atachuana na Slaven Bilic aliyetikisa vigogo Uingereza.
Everton ikiwa chini ya kocha mpya Ronald Koeman waliomng'oa Southampton ataikaribisha Tottenhman Hotspurs katika uwanja wa Goodson Park ambapo mchezo huo unawakutanisha makocha walipita kuinoa Southampton siku za hivi karibuni.
Bournemouth wataikaribisha Manchester united kwenye uwanja wao wa nyumbani ikiwa ni siku chache tangu Mourinho 'the special one' apate kibarua kwa mashetani hao wa Old Trafford hamu ya mshabiki wa Manchester united ni kuiona united mpya chini ya kocha huo.
Claudio Ranieri akiwa na Leicester city atakanyanga ardhi ya Hull city katika mchezo wa ufunguzi kuchuana na mkongwe mwenzie aliyeipandisha tena daraja timu ya Hull city Steve Bruce ambapo hamu ya wengi ni kuona ujio na makali ya bingwa huyo mtetezi.
Mechi zingine zitakazochezwa katika wiki ya ufunguzi ni pamoja na Manchester city v Sunderland, Middlesbrough v Stoke, Southampton v Watford, Crystal Palace v Westbrom pamoja na Burnley dhidi ya Swansea.

Comments
Post a Comment