Aliyekuwa kocha kocha wa Azam Mcameroon Joseph Marius anatarajiwa kuwasili Tanzania kumalizia mazungumzo ya mwisho kuhusiana mpango wa kuinoa Simba.
Simba inataka kumpa Omog mkataba wa mwaka mmoja baada ya kufikia makubaliano kwa njia ya simu na barua pepe na hivyo kocha amekubali kuja Dar es Salaam.
Simba itakuwa timu ya pili kunolewa na kocha huyo baada ya kufanya hivyo akiwa na Azam ambayo aliinoa kwa msimu mmoja na nusu lakini aliondolewa baada ya Azam kushindwa kufikia malengo yao.
Mwalimu aliwahi kuipa kombe la shirikisho timu ya FC Leopard ya Congo Brazaville mwaka 2014 wakati anaifundisha timu hiyo ikiwa moja ya mafanikio aliyopata akiwa kama mwalimu wa soka.
SOURCE: BIN ZUBEIRY

Comments
Post a Comment