Kocha wa timu ya taifa ya jamhuri ya watu wa Ireland Martin O'Neill amesema kuwa timu yake itashambulia kwa nguvu katika mechi dhidi ya Ufaransa inayochezwa leo.
Kocha huyo wa zamani wa timu ya Aston Villa alisema hana sababu ya kuigopa Ufaransa na kufanya mashambulizi ya kustukiza badala yake timu yake itacheza mpira mwingi bila kuogopa makali ya wenyeji hao wa mashindano.
"Tulicheza vizuri dhidi ya Sweden, tulipigana na kushinda dhidi ya Italy ingawa tulipoteza dhidi ya Ubelgiji wao wanatuzidi, lakini timu yangu itashumbulia kwa nguvu dhidi ya Ufaransa." Alisema kocha huyo.
Ireland itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kudhulumiwa goli dhidi ya Ufaransa baada ya Thienry Henry kufunga kwa mkono katika mchezo wa kufuzu fainali za kombe la dunia nchini Afrika kusini mwaka 2010, katika mchezo uliochezwa Novmber 18, 2009.

Comments
Post a Comment