Katika moja ya mipango ya kuimarisha timu ya Manchester united kocha wa timu hiyo Jose Mourinho ameweka mpango wa kumsajili Aaron Ramsey.
Mourinho anajiandaa kuweka mezani dau la paundi 50 milioni ili kuwaishawishi Arsenal imwachie kiungo huyo machachari ambaye anatamba kwenye ardhi ya Emirates.
Ramsey amekuwa moja muhimili mkubwa kwa sasa kwenye Arsenal na hivyo Mourinho anavutiwa na huduma ya mchezaji kwenye ardhi ya Old Trafford.
Ramsey 25, kwa sasa anaitumikia timu ya taifa ya Wales ambayo ipo kwenye machuano ya EUFA euro inayoendelea nchini Ufaransa wakingoja kuendelea na hatua ya 16 bora.

Comments
Post a Comment