Redmond akaribia kutua Southampton


Mchezaji wa timu ya Norwich Nathan Redmod anakaribia kutua Southampton baada ya kuwasili kwenye timu hiyo kukamilisha zoezi la kufanyiwa vipimo leo.

Southampton inataka kukamilisha usajili wa mchezaji huyo ili kuziba pengo la Sadio Mane ambaye huenda akatua Liverpool kutokana na mazungumzo baina timu hizo mbili kuendelea vizuri baada ya Liverpool kukubali kulipa dau la euro 30 milioni.

Winga huyo wa Norwich atatua Southampton kwa dau la paundi 11 milioni baada ya kuitumiki Norwich kwa miaka 3 akitokea Birmingham city mwaka 2013.

 

Comments