Pamoja na kushuka kiwango kwa mchezaji wa Liverpool Mario Balotelli lakini timu ya Sampdoria inahitaji kumsajili mchezaji huyo.
Balotelli ameshindwa kuwika tangu asajiliwe na Liverpool kwa dau la euro 16.5 milioni baada ya kufunga goli moja tu kwenye ligi ya England.
Licha ya kushuka kiwango lakini timu ya Sampdoria inavutika na mpango wa kumsajili mchezaji huyo ambaye hana maisha ya uhakika Anfield na baada ya kufanya vibaya AC Milan alipokuwa kwa mkopo.
Sampdoria inamtaka Mario Balotelli apunguze kiasi cha euro 4 milioni cha mshahara anachotaka kulipwa kwa mwaka ili wakamilishe dili hilo.

Comments
Post a Comment