Sanchez mchezaji bora Copa America


Mshambuliaji wa timu ya taifa ya chile Alexis Sanchez ameibuka kuwa mchezaji bora wa michuano ya Copa America timu yake ikitwaa ubingwa.

Chile waliiondoa Argentina kwa mikwaju ya Penati na kuwafanya wapoteze kwa fainali ya pili mfululizo kwenye michuano hiyo baada ya mabingwa hao kutetea taji hilo.

Sanchez alifunga magoli mawili katika mashindano hayo na kutoa pasi tatu za magoli kiwango bora alichokionesha mchezaji huyo kinamfanya kuwa kinara na mchezaji bora wa mashindano.

Licha ya Sanchez kuumia lakini alijikaza hadi kocha wa timu hiyo alipoamua kumtoa mchezaji huyo zikiwa zimesalia dakika 15 kumalizika kwa mpira kwenye muda wa nyongeza (extra time) wa dakika 30.

Comments