Serengeti boys kuingia kambini Juni 13


Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 'Serengeti boys' kujiandaa na mchezo wa kufunzu kombe la mataifa Afrika kwa vijana dhidi ya Shelisheli.

Serengeti itashuka dimbani dhidi ya Shelisheli Juni 25 mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa kugombea tiketi nyumbani ambapo ule wa Marudiano utachezwa Julai 2 mwaka huu.

Timu hiyo ya vijana ilifanya ziara nchini India kushiriki michuano ya kimataifa ya vijana ambayo yanatambuliwa na FIFA ( AIFF International Youth Tournament 2016) ikiwa sehemu ya kuiandaa na kuimarisha timu hiyo kwa mashindano ya kimataifa.

Licha ya kutoka katika Ukanda usiovuma kimpira ndani ya Afrika Mashariki Serengeti Boys iliweza kucheza mfululizo michezo saba za kimataifa bila kufungwa dhidi ya Misri, Korea, India, Malaysia na Marekani hali iliyopelekea timu hiyo kupokea mialiko mbalimbali ya mechi za kirafiki duniani.

Comments