Shearer aitaka England


Mshambuliaji wa zamani wa timu  England Alan Shearer yupo tayari kumrithi Roy Hodgson na kuwa kocha mpya wa England.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Blackburn na Newcastle alisema kuwa England ilimnyima kazi miaka mitano iliyopita kutokana na kukosa uzoefu lakini ana imani kwa sasa yupo kamili.

Shearer na Steve McClaren ambaye pia ni kocha wa zamani wa England alilalamikia suala zima la ukosefu wa mbinu kwa kocha Roy Hodgson jambo lililopelekea England kutupwa nje ya mashindano mapema.

Shearer aliwahi kufanya vizuri akiwa na Blackburn pamoja na Newcastle na moja kati ya wafungaji wa muda wote kuwahi kutokea nchini England.

Comments