Simba kufanya kweli Malawi


Timu ya Simba imeanza kufanya mazunguzo ya kumsajili beki wa Black Leopard ya Afrika Kusini pamoja na timu ya taifa ya Malawi Harry Nyirenda.

Beki huyo ameiongoza timu ya Malawi kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Zimbabwe ambapo katika mchezo huo aliyekuwepo mwenyekiti wa kamati ya usajili Simba Zacharia Hans Poppe.

Hans Poppe alifika kwenye uwanja huo kumwangalia beki huyo na kufanya naye mazungumzo ikiwa ni moja ya mipango ya Simba kuimalisha Ukuta wake msimu ujao.

Mbali na usajili wa beki huyo mwenyekiti huyo wa Simba yupo kwenye zoezi la kukamilisha mpango wa kupata kocha mpya atakaye kinoa kikosi cha Simba msimu ujao.

Comments