Uongozi wa Simba huenda ukamleta mshambuliaji wa Burundi Laudit Maugo baada ya kumkosa mchezaji huyo msimu uliopita.
Mavugo amemaliza mkataba wake na Vital O' na sasa kazi imebaki kwa wana msimbazi hao kuhakikisha mshambuliaji huyo anayetisha kwa kufumania nyavu anatua Simba.
"Ni kweli tunampango wa kumleta Mavungo na huenda akatua muda wowote kuanzia sasa." Kilisema chanzo.
Simba imesajili wachezaji wanne wa ndani na sasa inaangalia uwezekano wa kuleta nyota wa kigeni ili kuongeza nguvu kwenye timu yao.

Comments
Post a Comment