Simba yapata jembe, asaini miaka 2


Timu ya Simba imekamilisha usajili wa kiungo wa timu ya Mtibwa Sugar Muzamil Yasin ambaye amesaini miaka miwili kwenye timu hiyo.

Simba inahaha kukamilisha dili la Shiza Kichuya baada ya kufanikisha hilo la Muzamili Yasini ambao wote wanatoka timu moja.

Kusaini kwa mchezaji huyo kunaifanya Simba kukamilisha usajili wa wachezaji watatu baada ya ule wa beki Emanuel Semwanza na Kiungo Jamal Mnyate wote kutoka Mwadui.

Hata hivyo bado Simba haijataka kuwa wazi juu wa  wachezaji inayotaka kuwasajili lakini isadikika timu hiyo ipo kwenye mpango wa kumsajili Jeremia Juma na Kimwenya wa Prisons.

Comments