Simba yasajili mwingine Mtibwa


Timu ya Simba imeonesha kwamba imezamilia kufanya kweli msimu ujao baada ya kukamilisha usajili wa kiungo wa Mtibwa Mohamed Ibrahimu.

Kiungo huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu ya Simba na sasa anakuwa mchezaji w pili kusajiliwa na Simba kutoka Mtibwa.

Kiwango bora kinachooneshwa na kiungo huyo ndio kimepelekea kamati ya usajili ya Simba kuchukua maamuzi ya kumsajili mchezaji.

Kuondoka kwa Mohamed Ibrahimu kumekamilisha idadi ya wachezaji watano akiwemo Adrew Vicent ambaye alitimkia Yanga.

Comments