Stars yamchelewesha kichuya simba


Kiungo mshambuliaji wa timu ya Mtibwa sugar Shiza kichuya amesema kuwa kuingia kambini na Taifa Stars kumechelewesha kukamilika kwa dili lake na Simba.

Inasadikika kiungo huyo wa Mtibwa alisaini mkataba wa awali na Simba lakini sasa yupo kambini na timu ya taifa ambayo inajiandaa na mchezo wa kufuzu kombe la mataifa Afrika dhidi ya Misri kesho.

Kichuya alisema amemalizana na Simba mambo binafsi lakini dili hilo limesitishwa kwanza kutokana na ratiba ya Taifa Stars inayowakali dhidi ya Misri.

Simba bado inaendelea na mchakato wake wa kusajili nyota mbalimbali ambao wataokoa jahazi kwa timu hiyo ambayo haijafanya vizuri kwa miaka minne sasa.

Comments