Aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Nigeria 'super eagles' Steve Keshi amefariki dunia ghafla siku ya leo.
Taarifa za ndani za habari kutoka nchini humo zimeripoti kuwa Keshi 54, amefariki kutokana na shambulio la moyo ikiwa ni wiki moja baada ya kumzika mkewe.
Keshi ameingia kwenye historia akiwa na rekodi ya kutwaa ubingwa wa mataifa Afrika akiwa mchezaji wa timu ya taifa ya Nigeria mwaka 1994 na kuingoza nchi yake kutwaa ubingwa huo 2013 nchini Afrika kusini akiwa kama kocha.
Licha ya kuinoa Nigeria mchezaji huyo wa zamani wa Anderlecht amewahi kuinoa timu ya taifa ya Mali na Togo.
Kocha huyo alinyimwa mkataba mpya wa kuingoza Nigeria baada ya kushindwa kufuzu kwenye michuano ya kombe la mataifa Afrika mwaka 2015 na kuondolewa kwenye nafasi ya uangalizi wa timu hiyo baada ya aliyekuwa raisi wa Nigeria Jonathan Goodluck kuingilia kati suala lake.

Comments
Post a Comment