Tambwe, Ngoma wamwondoa Nonga Yanga


Mshambuliaji Paul Nonga ametimka katika timu ya Yanga na kurejea tena Mwadui FC kwa mara nyingine.

Uwepo wa Donald Ngoma na Amis Tambwe umemwondoa Nonga kwenye timu ya Yanga baada ya kukosa baada ya kukosa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza kutokana na washambuliaji hao kuwa moto.

Paul Nonga aliiandikia Yanga barua ili aweze kuondoka kwenye timu hiyo kutokana na kushindwa kufua dafu mbele ya Donald Ngoma na Amisi Tambwe

Licha ya Nonga kurejea tena mwadui lakini haifahamika rasmi kama mchezaji huyo ameuzwa moja kwa moja au amerejea kwa mkopo.

Comments