Telela atemwa Yanga


Timu ya Yanga imemwacha kiungo Salum Telela baada ya kumnyima mkabata mpya wa kuendelea na mambingwa hao.

Hivi karibuni Yanga iliwaongeza mikataba baadhi ya wachezaji wa ndani na wa nje ya Tanzania lakini haikufanya hivyo kwa Salum Telela ambaye kulingana na maamuzi ya mwalimu Hans Pluijm timu hiyo imeamua kuachana nae.

Timu hiyo pia imemtoa kwa mkopo golikipa wao Benedictor Tinocco na kumruhusu Paul Nonga kumtimka baada ya kuwasilisha barua ya maombi ya kuondoka kwenye timu hiyo mchezaji huyo aliyeigharimu Yanga shilingi milion 20 za Tanzania.

Simba ilikuwa inahusishwa kwenye usajili wa Salum Telela huenda ikafanya mpango wa kumsajili mchezaji huyo baada ya kuachwa na mahasimu wao.

Comments