Townsend azitoa macho Liverpool, City


Timu ya Liverpool na Manchester city ya England zote zinavutiwa nna mpango wa kumsajili winga Tottenham Hotspurs Adros Towsend.

Townsend mwenye thamani ya euro 12 milioni hayupo kwenye mipango ya kocha wa sasa wa Spurs Mauricio Pochettino na huenda akatimka kwenye timu hiyo.

Mchezaji huyo anaziingiza vitani Liverpool na Manchester city baada ya wote kuwaka nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo ambaye pia anafukuziwa na West Ham pamoja na Crystal Palace.

Townsend amewahi kufanya vizuri akiwa na Tottenham, Newcastle pamoja na timu ya taifa ya Uingereza licha ya kutoswa na kocha hiyo Roy Hogson kwa sasa.

Comments