Vardy aipotezea Arsenal


Mshambuliaji wa timu ya Leicester city na England Jamie Vardy amevunja rasmi ndoto za Arsenal baada ya kukubali dili la miaka minne kwenye timu yake.

Vardy atasaini mkataba mpya na timu yake baada ya kumalizika kwa kampeni za England kwenye michuano ya UEFA euro inayoendelea nchini Ufaransa.

Awali Arsenal ilitenga ofa ya euro 20 milioni na mshahara wa euro 120,000 kwa wiki ili kumshawishi mshambuliaji kutua Arsenal kwa ajili ya kuimarisha safu ya ushambuliaji.

Hata hivyo Ranieli aliamua kuweka ofa ya mshahara mpya wa euro 100,000 wiki ambao hautofautiani sana na ule wa Arsenal sasa Vardy 2, ameamua kujifunga rasmi Leicester.

Comments