Mshambuliaji wa Leicester city Jamie Vardy huenda akakamilisha dili lake la kutua Arsenal kabla ya kutua Ufaransa kwenye michuano ya EUFA euro.
Arsenal imekubali kulipa kiasi cha euro 20 milioni kama ada ya uhamisho wa mchezaji huyo baada ya kufanya makubaliano na Leicester city.
Mipango ya usajili ya mchezaji huyo inaweza kukamilika kabla timu ya England haijatua nchini ufaransa siku ya jumatatu heunda dili hilo likakamilika leo.
Wenger anataka kufanya mageuzi makubwa katika kikosi chake msimu ujao akiwa na mipango ya kusajili nyota kadhaa wenye majina ili kukabiliana na ushindani wa England 2016/17.

Comments
Post a Comment